Hatimae ngasa anko arejea Yanga

Baada ya kuenea kwa tetesi mbaimbali zikidai kuwa club ya Yanga SC sasa wameyumba kiuchumia kiasi cha kushindwa kufanya usajili wa nafasi tatu za wachezaji watakaoongeza nguvu katika kikosi cha Kombe la shirikisho Afrika.

Jumatano ya May 30 2018 kutoka mtandao wa habari za michezo wa shaffihdauda.com zimeripotiwa taarifa za kufanya usajili wa mshambuliaji wao wa zamani Mrisho Khalfan Ngassa, Yanga imemsajili Mrisho Ngassa kwa ajili ya kuongeza nguvu.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri Mrisho Khalfan Ngassa aliwahi kuichezea Yanga kwa miaka kadhaa kabla ya kuamua kwenda Free State ya Afrika Kusini, Fanja FC ya Oman, Mbeya City ya Mbeya na baadae akajiunga na Ndanda FC kabla ya leo hii kutangazwa kurudi Yanga.

MaoniMaoni Yako