Harmonize, Mr Flavour na Yemi Alade Kuliamsha Dude


Mwaka 2018 unaweza ukawa ni wa neema kwa Harmonize. Msanii huyo ameonyesha ngoma nyingine ambayo amefanya na wasanii wakubwa wa Nigeria.

Harmonize kupitia mtandao wa Instagram ameweka video fupi ukisikika wimbo huo ambao ndani yake zinasikika sauti za Mr Flavour na Yemi Alade.

Hata hivyo haijafahamika kama wimbo huo ni wa msanii huyo wa WCB au ameshirikishwa.

Kwa sasa Harmonize anafanya vizuri na ngoma yake ya Kwa Ngwaru ambapo video ya wimbo huo imetazamwa zaidi ya mara milioni tisa kwenye mtandao wa YouTube.
Credit: Udaku Special
MaoniMaoni Yako