Harmonize Afurahishwa na Mapokezi Airport Mwanza


Msanii wa Bongo flava kutoka WCB Harmonize amewasili jijini Mwanza kwa ajili ya uzinduzi wa Mashindano ya Miss Mwanza na Lake zone.

Harmonize na mkewe wamefurahishwa na mapokezi hayo na kuwaomba mashabiki  wasikose kwani wamewandalia vitu vipya.

Harmonize anayetamba na kibao cha Kwangaru aliyemshirikisha Rais wa WCB Diamond, ameambatana na mkewe Sarah, na kupokelewa na baadhi ya washiriki wa mashindano ya Miss Mwanza.

Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Mepal Management Wakala wa Miss Mwanza 2018 , yanatarajia kuzinduliwa Mei 12 kwenye viwanja vya Rock City Mall.
Credit: Udaku
MaoniMaoni Yako