Harmonize afunga ndoa kisiri siri na Sarah

Staa anayetamba na wimbo Kwangar, Harmonize amebainisha kuwa amefunga ndoa  na mpenzi wake Sarah Michelotti ingawa hakupenda kuliweka wazi kwa kuwa anaamini ndoa inapaswa kutambulika kwa Mungu.
Akizungumza na mwandishi wa Gazeti dada la Mwananchi, Nation la nchini Kenya, Harmonize alikiri kufunga ndoa kwa siri akisema kuwa hawezi kueleza zaidi kwa kuwa walishaamua iwe hivyo.
“Ndio tumefunga ndoa. Si lazima kutangaza unapoamua kuchukua uamuzi kama huo. Naamini Mungu pekee akifahamu inatosha,” anasema Harmonize.
Akizungumzia kuhusu ujauzito wa mpenzi wake huyo ambao  waliutangaza mwanzoni mwa uhusiano wao anasema uliharibika.
Siku za hivi karibuni Harmonize aliingia katika malumbano katika mitandao ya kijamii na aliyekuwa mpenzi wake, mwigizaji Jackline Wolper baada ya kumtuhumu kuwa analelewa na mwanamke huyo mwenye asili ya Italia.
Mwandishi wa Nation, Thomas Matiko alipomuuliza iwapo amemuoa Sarah kwa kuwa anatoka katika familia yenye fedha, Harmonize alisema: “Kila mtu ana uhuru wa kuongea, wataongea sana lakini najua nampenda mke wangu na ninafurahia maisha
MaoniMaoni Yako