Gor Mahia chali kwa Hull City, wapigwa 4-3 kwa penaltiNairobi. Licha ya kuonesha mchezo mzuri katika dakika zote 90 za mchezo wa kirafiki iliyopewa jina la Hull City Challenge, mabingwa wa soka nchini, Gor Mahia, wameshindwa kuwatambua Wazungu wa Hull City nyumbani.


Kogalo ambao walitawala mechi hiyo iliyomalizika muda mfupi uliopita kwenye uwanja wa Kasarani Jijini Nairobi, kwa asilimia 57 dhidi ya 43 za Hull City, walijikuta wakilazimishwa sare 0-0 baada ya dakika 90 kabla ya kupigwa 4-3 kwa mikwaju ya penalti.


Katika mtanange huo uliosubiriwa kwa hamu, Kogalo walionesha kiwango kizuri huku kiungo wake Mchezeshaji, Francis Kahata, akiwapeleka puta 'wazungu' hao kabla ya kutolewa katika dakika ya 86 na nafasi yake kuchukiliwa na Boniface Omondi.


Hull City nao hawakuachwa Nyuma, kwani katika dakika 10 za mwanzo, walifanya mashambulizi mfululizo langoni mwa wenyeji, ambapo kama sio uimara na wepesi wa nahodha Harun Shakava, kumpokonya mpira, Straika wa zamani wa Man United, Fraizer Campbell, mambo yangeharibika.Katika hatua ya kupiga penalti, mlinda lango wa Gor Mahia alionesha umahiri wake baada ya kudaka mikwaju mitatu ya wapigaji wa Hull City, lakini juhudi zake hazikuweza kuiokoa Kogalo ambao walikubali kichapo cha 4-3.


Wakati huohuo, Gavana wa Machakos, Dk alfred Mutua, ambaye awali aliahidi zawadi ya shilingi 500,000 kwa Kogalo endapo wataifunga Hull City, ametoa shillingi 300,000 kwa klabu hiyo licha ya kupata kichapo.
Credit: Mwanaspoti
MaoniMaoni Yako