Gavana wa Machakos aahidi neema Gor wakiifunga Hull City

Gavana wa kaunti Machakos, Alfred Mutua amewapa motisha wachezaji wa Gor Mahia, wanaopambana na Hull City ya England katika mechi ya kirafiki, muda huu katika uwanja wa Kasarani Jijini Nairobi.
Kupitia akaunti yake ya Twitter Gavana huyo ambaye amewahi kuwa msemaji wa Serikali, amekimwagia sofa kikosi cha Kogalo, huku akiahidi kuwapa shilingi laki tano (Ksh 500,00), endapo watafanikiwa kuitandika Hull City.
"Kama haujawahi kuishuhudia Gor Mahia, ikicheza huwezi waelewa kiwango chao, Hawa jamaa ni mafundi. Ninawasapoti na naahidi wakishinda leo, waje wachukue 500, 000
Kipindi cha pili kimeanza, ambapo milango ya timu zote bado ni migumu. Mechi hii imeandaliwa na Sportpesa kwa ushirikiano na shirikisho la soka nchini FKF, na kuhudhuriwa na waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga
Credit: Mwanaspoti
MaoniMaoni Yako