"From Hero to Zero" Hiki ndicho kiingilio Kuiona Yanga dhidi ya Rayon Leo Juma tano

Yanga ina kibarua cha mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika leo Jumatano saa 1 jioni dhidi ya Rayon Sports.

Viingilio vya mechi ya Yanga dhidi ya Rayon Sports vimetangazwa na klabu hiyo itakuwa Sh3,000 kwa jukwaa la mzunguko huku VIP A kiwa ni 15,000 wakati VIP B na C itakuwa Sh 7, 000.
Hata hivyo wakati Yanga ikiwa na kibarua cha mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika leo Jumatano saa 1 jioni dhidi ya Rayon Sports, wachezaji kadhaa ikiwemo nyota wataukosa mchezo huo.

Yanga inashuka Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kucheza mechi hiyo ya pili katika hatua ya makundi ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza dhidi ya USM Alger ambao waliondoka vichwa chini uwanjani baada ya kutandikwa mabao 4-0 huko Algiers, Algeria.

Uhakika wa wachezaji ambao watakosekana kwenye mtanange huo ni Amis Tambwe ambaye bado hajaimarika vizuri kiafya, Donald Ngoma pia Beno Kakolanya ambaye alijitonesha goti lake katika mechi ya ligi dhidi ya Tanzania Prisons.
Mbali na hao yupo Ibrahim Ajib aliye na matatizo ya kifamilia, Papy Kambamba Tshishimbi aliyesafiri kurejea kwao kutokana na matatizo ya kiafya kwa ajili ya matibabu.

Wakati huo mchezaji Said Makapu atakuwa nje ya dimba kutokana na adhabu ya kuwa na kadi mbili za njano zitakazomfanya awakose Rayon Sports.

Source: Mwanaspoti
MaoniMaoni Yako