Faiza: Nampenda Sugu Ila Sio Kimapenzi


Muigizaji Faiza Ally ambaye ni mzazi mwenzie na Mbuge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, amedai kuwa bado anampenda Sugu ila hana hisia naye za kimapenzi kutokana na kile kilichotokea kati yao.

Hata hivyo Faiza amesema licha ya yote yaliyotokea kati yao mapenzi yake ya kweli kwa Sugu hayajawahi kuisha.

“Hisia na mapenzi ni tofauti, kwa sababu nampenda mapenzi ya kweli hayajawahi kufutika, i will always love him na kumpenda haina maana kuwa nina hisia naye. Nampenda ni ndugu yangu, baba watoto wangu,” Alifunguka Faiza Jumapili Katika Mahojiano Bongo5

Faiza na Sugu wamejaliwa mtoto kupata mtoto mmoja, Sasha. 
MaoniMaoni Yako