Emery atangazwa rasmi kocha Arsenal


ARSENAL imemtangaza rasmi aliyekuwa Kocha wa PSG, Unai Emery, kurithi mikoba ya Arsene Wenger Emirates.
Emery anakuwa kocha wa pili kuinoa Arsenal akitokea nje ya Uingereza, baada ya Wenger.
Baada ya kumthibitisha kocha huyo raia wa Hispania, Mkurugenzi Mkuu wa Arsenal, Ivan Gazidis, alisema “Unai Emery alikubalika na wengi kuanza ukurasa mpya wa historia ya Arsenal”.
Emery, 46, amejiunga na 'The Gunners' baada ya kuibebesha ubingwa wa Ligue 1 PSG.
Mhispania huyo alitwaa ubingwa wa ndani mara nne na miamba hiyo ya Ufaransa huku hivi karibuni kabla ya kutua PSG, akiibebesha Sevilla Kombe la Europa League mara tatu mfululizo.
"Unai ana rekodi nzuri ya mafanikio, ameendeleza baadhi ya makinda wenye vipaji Ulaya na kuweza kucheza soka la kuvutia, ana mfumo wa maendeleo kisoka ambao ni sahihi kabisa kwa Arsenal," Gazidis aliongeza.
Emery atakuwa na jukumu kubwa la kuanza ukurasa mpya Arsenal kufuatia Wenger, 68, aliyeondoka kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara tatu na Kombe la FA mara saba.
"Ni mwenye furaha kupewa majukumu ya kuanza ukurasa huu mpya katika historia ya Arsenal," alisema Emery.
"Ninafuraha kujiunga na moja ya klabu kubwa katika mechi. Arsenal inapendwa kote duniani kupitia mfumo wake wa uchezaji, kuwajali wachezaji makinda, uwanja mzuri na namna klabu inavyoendeshwa.
"Nina msisiko kuhusu kila tutakachokifanya pamoja na ninatazama mbele kuleta upendo kwa kila mmoja Arsenal sambamba na nyakati nzuri na kumbukumbu."
Credit: IPP Media
MaoniMaoni Yako