EBITOKE: Wanja umenipa maisha

Annastazia Exavery ‘Ebitoke’
MSANII wa vichekesho, Annastazia Exavery ‘Ebitoke’ amesema kuwa wanja mwingi ‘anaojisiriba’ machoni ndio umempa maisha na kutimiza ndoto zake za muda mrefu.

Akizungumza na gazeti hili, Ebitoke alisema kuwa habari ya kufanya ‘make up’ ameshaisahau kabisa kwani wanja ndio kitambulisho chake kikubwa siku asipoupaka na kuamua kujiremba anasahaulika kabisa.


“Ninauheshimu sana wanja kwani ndio umenipa maisha hata akaunti yangu ya benki inasoma vizuri na nimetimiza ndoto zangu nyingi tu japokuwa watu wengi watakuwa hawauelewi huu wanja,” alisema Ebitoke.
MaoniMaoni Yako