Dongo la haji manara kwa Yanga


Uongozi wa klabu ya Simba kupitia Ofisa Habari, Haji Manara, amefunguka kwa kusema kuwa walitolewa katika mashindano ya kimataifa kwa heshima baada ya kishindwa kufungwa mchezo hata mmoja.

Manara ameeleza hayo huku akijitofautisha na Yanga ambao jana walikuwa kibaruani kukipiga na Rayon Sports ya Rwanda kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Msemaji huyo wa Simba amefunguka kwa kusema kuwa Simba iliondolewa kwa heshima tofauti na watani zao wa jadi ambao wamekuwa hawafanya vizuri huku akigusia kichapo cha mabao 4-0 walichokipata dhidi ya USM Alger.

Haji alishindwa kuwatakia kheri Yanga hapo jana alipoitisha kikao na waandishi wa habari akisema hana muda huo na badala yake anahusika na Simba pekee.

Simba itakuwa ina kibarua Jumamosi ya wiki hii kukipiga na Kagera Sugar katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, mchezo wa ligi kuu bara.

Source: Saleh Jembe

MaoniMaoni Yako