Devotha aanguka, atenguka mguu

MUIGIZAJI wa sinema za Kibongo, Devotha Mbaga amepata janga baada ya kuteleza na kutenguka mguu wake.
Akizungumza na Amani kwa njia ya simu juzi, Devotha alisema alipata tatizo hilo hivi karibuni nyumbani kwake, Kigamboni jijini Dar alipokuwa anataka kupanda kwenye gari lake.
“Nilianguka mguu ukateguka, nashukuru Mungu naendelea vizuri kwani nilikwenda hospitali ya Vijibweni Kigamboni na kutibiwa. “Nimepewa gongo ambalo natembelea pia niliambiwa tatizo limetokana na mishipa yangu ya miguu imevimba lakini sasa hivi naendelea vizuri,” alisema Devotha.
Credit: Global Publishers