Saturday, May 26, 2018

Chris Brown amkosesha usingizi mrembo huyu wa Bongo

Tags


MUUZA nyago kwenye video mbalimbali za wanamuziki Bongo, Irene Hilary ‘Lynn’ ambaye aliwahi kusumbua kwenye vyombo vya habari akidaiwa kutoka na mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ amefunguka jinsi anavyomzimia kimahaba mwanamuziki wa Marekani, Chris Brown.

Lynn alisema kuwa ametokea kumpenda sana mwanamuziki huyo kiasi ambacho haelewi atafanyaje ila anaomba katika maisha yake siku moja akutane naye, amueleze hisia zake.

“Hivi ulishawahi kumpenda mtu mpaka ukawa huelewi sababu? Sasa ndio mimi nilivyo kwa Chris, naamini siku nitaonana naye na kama ikitokea hivyo kwa kweli nitamfikishia hisia zangu, kama atakubali au kukataa, niwe tu nimemuambia, naamini nitakuwa na amani,” alisema Lynn.