Chemical: Nilitongozwa Sana Baada ya Kutamka Hadharani Kwamba Mimi ni Bikra

Msanii wa muziki nchini, Claudia Lubao, maarufu kama Chemical amesema kwamba kitendo cha msichana kuwa bikra sio kitu kibaya cha kuonea aibu bali ni jambo zuri na inategemea mtu amekulia katika mazingira gani.

Chemical amesema hayo jana  Mei 30, 2018 wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha Kikaangoni cha   EATV, ampapo aliongeza  kuwa kitendo cha msichana kuwa bikra au kutokuwa bikra ni uamuzi binafsi.

“Kuna wasichana mpaka leo hii wanaenda kuolewa bado wapo bikra na ni wazuri, kwahiyo kuwa na ubikra sio ushamba, kutokuwa na bikra sio ushamba inategemea umekulia wapi, kwahiyo kila mtu yupo vile alivyo kutokana na alikopitia” amesema Chemical

Chemical ameongeza kuwa alifuatwa na wanaume wengi wakitaka kuanzisha uhusiano wa kimapenzi tangu aliposema hadharani kwanba yeye ni bikra.

"Mimi nilitongozwa sana niliposema kwamba ni bikra, nilifuatwa sana na watu wazima, kusema ukweli nilitongozwa sana nikaona kumbe kuwa na bikra ni dili”.

Msanii huyo amedai kwamba aliamua kuwa bikra kwa wakati ule kwasababu haukuwa muda sahihi kwake kuingia katika mahusiano ya kimapenzi.

by richard@spoti.co.tz
MaoniMaoni Yako