Cheki walichopanga yanga kumfanyia ngoma pindi mkataba ulipovunjwa


Na George Mganga

Licha ya kusikitishwa na maamuzi yaa aliyekuwa mchezaji wao, Mzimbambwe, Donald Ngoma kuondoka na kutimkia Azam FC kisha kusaini mkataba wa mwaka mmoja, uongozi Yanga umesema ulipanga kumpa mapumziko ya mwaka mmoja.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili na Maadili wa klabu hiyo, Hussein Nyika, ameeleza kuwa Yanga ilipanga kumpa mapumziko ya mwaka mmoja Ngoma ili aweze kutibiwa vizuri na hatimaye aweze kurejea Uwanjani.

Nyika ameeleza uongozi ulijipanga kwa ajili ya kufanya hivyo ili kumpa muda mzuri Ngoma wa kuweza kupata matibabu akiwa amepumzika ili hata akili yake kisaikolojia iweze kukaa vizuri.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya mchezaji huyo aliyekuwa kwenye matibabu kuandamwa na majeraha ndani ya msimu mzima wa 2017/18 kusajiliwa na Azam FC.

Tayari Ngoma ameshaijiunga na Azam na amesaini mkataba wa mwaka mmoja na wiki ijayo atapelekwa Afrika Kusini kufanyiwa vipimo vya afya kisha matibabu endapo vipimo vitaonesha ana matatizo kiafya.

Source: Saleh Jembe

MaoniMaoni Yako