Bodi Ya Ligi Yaanza Mazungumzo Mapya Na Vodacom


Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TPLB), imeeleza kuanza mazungumzo na wadhamini wake wakuu, Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom kwa ajili ya kuongeza nao mkataba.

Kwa mujibu wa Mkurungenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, Boniface Wambura, amesema tayari wameshaanza mazungumzo hayo ili Vodacom waweze kutia saini ya kuendelea kuidhamini Ligi.


Wambura amesema mkataba waliokuwa wameingia na Vodacom unamaliza baada ya msimu huu wa ligi unaohitimishwa Jumatatu ya wiki kesho, hivyo imeabidi waanze kuzungumza nao kuona kama wataweza kuongeza mwingine.

Vodacom wamekuwa wadhamini wakuu wa muda mrefu katika Ligi Kuu ambapo wamekuwa wakitoa kiasi cha shilingi milioni 80 kwa bingwa wa nchi.
MaoniMaoni Yako