Bill Nas akiri video yake na Nandy imemuharibia


MWANAMUZIKI wa Hip Hop Bongo, William Lymo ‘Bill Nas’, amefunguka kwamba video ya utupu inayomuonesha yeye na mwanamuziki Nandy, aliyewahi kuwa mpenzi wake bado inamtesa kwa sababu imeporomosha heshima yake kwa kiasi kikubwa.

Akichonga na Mikito Nusunusu, Bill Nas aliongeza kuwa wakati video hiyo inavuja alikuwa Dubai kwa ajili ya mapumziko ya sikukuu yake ya kuzaliwa na kabla ya hapo kuna vitu alikuwa amepanga kuvifanya baada ya kurudi nchini, lakini ameshindwa kufanya kutokana na video hiyo.

“Kiukweli ile video bado inanikosesha amani kwa maana kuna watu mpaka huwa naona noma ‘kuwaface’ nikifikiri waliiona video hiyo.

“Hata hivyo namshukuru Mungu watu wengi wameweza kunielewa hasa watu wangu wa karibu, ninafahamu hili nalo litapita,” alisema Bill Nas.
Credit: Udaku
MaoniMaoni Yako