Bifu la Diamond na Kiba nalifurahia sana – MpotoMwanamuziki Mrisho Mpoto maarufub ‘Mjoma’, amesema anatamani ‘uhasama’ uliopo kati ya Diamond Platnumz na Alikiba uendelee kuwepo daima.

Mpoto amesema uhasamu wao umekuwa wa manufaa katika muziki wa Bongo Fleva na burudani kwa ujumla na kwamba anaona wakipatana watapoteza ladha ya muziki huo wa Tanzania unaokuja juu.


“Yaani mwenzenu hilo bifu la Diamond na Kiba nalifurahia sana, limeleta utamu katika muziki, ninachoomba tu libaki katika soko la muziki na lisiwe lile la kushindwa hata kusalimiana.

Mpaka leo naamini wanaowatengenezea uadui ni mashabiki wa muziki wao kitu ambacho ni kizuri kinachowasaidia katika muziki wao”

amesema Mpoto aliyejikita katika kughani mashairi

Mkali huyo wa kibao cha ‘Nikipata Nauli’ amesema haoni sababu ya wawili hao kutoa nyimbo pamoja kwa kuwa wataharibu utamu mzima wa ushindani wao na kutaka wabaki hivyo hivyo.
MaoniMaoni Yako