Bayern Munich wataweza kupindua matokeo leo dhidi ya bayern?..

David Alaba anatarajia kurudi uwanjani hii leo baada ya kuwa majeruhi, Javi Martinez pia amesafiri na timu lakini hali ya Arjen Robben bado sio nzuri na hii imemlazimu kubaki Ujerumani wakati Bayern Munich wakisafiri kwenda Hispania.

Katika michezo ya nusu fainali saba iliyopita katika michuano ya Champions League hakuna timu ambayo imewahi kupindua matokeo ya kufungwa mabao 2-1 katika uwanja wao wa nyumbani.

Bayern Munich wanaonekana vibonde kabisa wa Real Madrid, katika mechi 6 zilizopita katika hatua ya mtoano Bayern Munich wamepoteza zote mbele ya Los Blancos na hii ikiwa idadi yao kubwa zaidi kupoteza dhidi ya timu moja katika Champions League.

Cristiano Ronaldo amefunga mabao 9 dhidi ya Bayern Munich, mchezaji pekee ambaye amefunga mabao mengi dhidi ya timu moja ya Champions League ni Cr7 mwenyewe ambaye ameifunga Juventus mabao 10.

Hakuna timu ambazo zimekutana mara nyingi katika Champions League kama Real Madrid na Bayern Munich, hadi hizi sasa wamekutana mara 26, Bayern Munich akishinda mara 11 huku Real Madrid akishinda 12.

Uwanja wa Santiago Bernabeu ndio mahala pachungu zaidi kwa wapinzani katika Champions League, katika dimba hilo Real Madrid wamefunga katika michezo yao 41 ya mwisho ya CL na mechi pekee waliyoshindwa kufunga ilikuwa dhidi ya Barcelona mwaka 2011.

Mbaya zaidi kwa Bayern Munich ni kwamba wanakwenda ugenini katika kipindi ambacho wamecheza michezo 13 ya Champions League ya ugenini na yote wameruhusu bao, huku mshambuliaji wao tegemezi Robert Lewandowski akiwa hajafunga katika mechi 4 zilizopita za CL.

Source: Shaffih Dauda
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz

MaoniMaoni Yako