Balaa la kadi nyekundu latua Kombe la DuniaShirikisho la Soka la Dunia (Fifa) limeangaza kanuni mpya zitakazotumika kwenye fainali za Kombe la Dunia kuanzia Juni14, ambapo wachezaji watatolewa nje na kulimwa kadi nyekundu hata kama mwamuzi hakuona tukio baada ya kulibaini hata kama muda ulipita.

Kanuni hizo za Kombe la Dunia zinaelekeza zaidi kwamba hata kama mchezo umeendelea na kulikuwa na makosa awali ambayo mwamuzi hakuyaona, ataruhusiwa kutoa adhabu hata kama ni kutolewa nje kwa mchezaji au wachezaji husika.

Kwa kanuni za sasa zinaeleza kwamba iwapo mchezo utakuwa umeshaanza na kulikuwa na tukio ambalo lilifanyika na mwamuzi hakuona, basi hatalitolea adhabu.

Kanuni hiyo imewekwa ili kuondoa matukio ya vurugu au adhabu ambazo mwamuzi hakuziona na zilistahli kutolewa adhabu.

Kanuni hiyo itakwenda sambamba na teknolojia ya VAR ambayo itatumika kwenye fainali za Russia za Kombe la Dunia.

Teknolojia hiyo ya VAR pia itatumika kwenye mechi zote za Kombe la FA msimu ujao, ambapo waamuzi watakuwa na mamlaka ya kutoa kadi hata baada ya kupata tahmnini ya tukio au mchezo.
MaoniMaoni Yako