Bado tunaikumbuka Everton- SportPesa

KAMPUNI ya Kubashiri ya SportPesa juzi imetimiza mwaka mmoja tangu ilipoanza uendeshaji wa shughuli zake za kibiashara nchini, wakati ilianzia rasmi Kenya mwaka 2014, kwa kishindo ikiwa imejizatiti katika kusaidia kukuza sekta ya michezo.
Katika kutimiza azma yake, SportPesa ilianza kwa kutoa mchango wa Sh. milioni 50 kusaidia maandalizi ya timu ya Serengeti Boys iliyokuwa ikijiandaa na michuano ya vijana ya AFCON iliyofanyika Gabon mwaka jana na baadaye iliingia mkataba wa udhamini wa miaka mitano kwa Simba, Yanga pamoja na mkataba wa mwaka mmoja na Singida United.
Udhamini huo ulishuhudia vilabu vya Simba, Yanga na Singida United vikishiriki michuano mipya ya SportPesa Super Cup ambayo ilikuwa na lengo na kumpata mshindi mmoja atakayechuana na klabu ya Everton.
Kwa takribani wiki moja (kuanzia Juni 5-11), kwenye Uwanja wa Uhuru ulifurika mashabiki lukuki waliokuja kushuhudia ladha ya michuano hiyo ambayo pia vilabu vya Gor Mahia, AFC Leopards, Tusker na Nakuru All Stars kutoka Kenya sambamba na Jang’ombe kutoka Zanzibar vikitoana jasho kuzisaka zaidi ya Sh. milioni 60.
Ziara ya Everton
Sote ni mashahidi jinsi SportPesa ilivyojitoa mhanga kuileta nchini klabu ya Everton ikiwa ni mara ya kwanza kwa klabu ya EPL kutembelea Tanzania na hivyo kuitangaza vyema nchi yetu kimataifa.
Sahau kuhusu mashabiki waliofurika uwanja wa Taifa Julai 13 kumshuhudia Wayne Rooney akivaa uzi wa Everton kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2004, dhidi ya Gor Mahia, lakini sote ni mshahidi jinsi ziara ile ilivyoleta manufaa makubwa.
Bajaji 120
Achilia mbali sekta ya michezo, lakini SportPesa pia imefanya promosheni za aina yake zilizokuwa na lengo ka kuinua kipato cha Mtanzania mmoja mmoja, ambapo ndani ya siku zaidi ya 170, Watanzania 120 wameweza kujishindia bajaji mpya aina ya TVS KING kila siku, kila wiki.
Sio rahisi kuilezea SportPesa kwa Makala moja kwani mambo ambayo wamefanya kwa kipindi cha mwaka mmoja ni mengi na makubwa.
Kwa niaba ya wapenda michezo wote nchini, tunapenda kuitakia kampuni ya SportPesa heri ya maadhimisho ya mwaka mmoja na hakika hatutaweza kuisahau ziara ya Everton, kwani ilimfumbua macho kila mmoja wetu na kuona kuwa kila jambo linawezekana kama tukiweka nia.
Credit: IPP Media
MaoniMaoni Yako