Baada ya mumewe kutajwa na Harmonize kwenye list ya waliotembea na Wolper, Shamsa akubali yaishe


Mugizaji wa Filamu Bongo, Shamsa Ford amesema hana bifu lolote na Harmonize mara baada ya muimbaji huyo kumtaja mume wake Chid Mapenzi katika orodha ya wanaume ambao alidai wamewahi kutoka kimapenzi na Jacqueline Wolper.

Muigizaji huyo amesema kuwa licha kutopendezwa na kitendo hicho kwa ujumla hana ugomvi na Harmonize ili maisha mengine yaendelee.

Soma Pia: Harmonize ataja list ya wanaume 12 waliotembea na Jacqueline Wolper

“Mume wangu ni mtu mpole sana, inawezekana hakupendezwa ila alikaa kimya, sisi wanawake tunamunkari ya hali ya juu, halafu unaona huyo kapata wapi huo ujasiri wa kuweka hivyo bila kufikiria hawa watu wengine tayari wana familia zao,” amesema.. Soma Zaidi
MaoniMaoni Yako