Baada ya Kupewa Onyo na TTF Haji Manara Akubali Yaishe

Kikao cha kamati ya saa 72 kilikaa na kujadili mambo mbalimbali ya Ligi hiyo sambamba na matukio yaliojitokeza, baada ya kukaa leo afisa mtendaji mkuu wa bodi ya Ligi Boniface Wambura alijitokeza mbele ya waandishi wa habari na kuzungumza maamuzi yaliofikia ikiwemo kumpa onyo kali msemaji wa Simba Haji Manara kwa kuingia uwanjani kushangilia wakati wa mchezo huo.

Baada ya kupewa onyo  Haji Manara aliandika hivi katika ukurasa wake wa instagram “Muungwana akivuliwa nguo huchutama..naomba radhi bodi ya ligi,TFF na wadau wote..nilihemewa na furaha ndugu zangu..hakuna raha kwangu mm na kwa mshabiki kama kumgalagaza mtani…it will never happen again..ila sijui itakuwaje siku ya kukabidhiwa mwali😁😁😁 @tanfootball #bodiyaligi 🙏🙏“ 
Chanzo: Udaku Specially