Azam yazidi kusalia nafasi ya pili, yaitwanga Majimaji 2-0


Kikosi cha Azam FC kimeendelea kukalia nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Majimaji FC, mchezo uliopigwa Uwanja wa Azam Complex.

Mabao katika mchezo yamefungwa na Frank Domayo pamoja na Shaaban Idd.

Matokeo hayo yanaifanya Azam ifikishe jumla ya pointi 52 ikiwa imecheza michezo 28 katika nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi.

Azam inaiombea Azam izidi kufanya vibaya ili iendelee kusalia kwenye nafasi hiyo, lakini endapo Yanga itashinda mechi zake zote zilizobaki, Azam itashuka chini na itarejea kwenye nafasi ya tatu.

Azam ipo mbele kwa zaidi ya michezo mitatu dhidi ya Yanga ambayo itashuka kucheza na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro Mei 13 2018.
Credit: Saleh Jembe
MaoniMaoni Yako