Amekununia na hataki kuzungumza na wewe? Fanya hivi!!KWA watu waliopo katika uhusiano wa kudumu, watakubaliana na mimi kwamba kuna wakati huwa inatokea mwenzi wako, na hii inawahusu zaidi wanawake, anaamua tu kukununia, ha­taki kuzungumza chochote na wewe.

Kila unachomuuliza anakujibu kwa mkato kisha anaendelea na mambo yake, hataki kushirikiana chochote na wewe na hata haki yako ya msingi huipati! Wengine huweza ku­dumu kwenye hali hii kwa muda mrefu na kama usipokuwa makini, hii inaweza kuwa sababu itakayowaingiza kwenye matatizo makubwa zaidi.

Bahati mbaya ni kwamba ni wanaume wachache sana wanaoelewa nini cha ku­fanya inapotokea mwanamke unayeishi naye, au unayempenda sana anakubadi­likia kiasi hiki. Yaani unamuona kabisa hayupo sawa, hakuchangamkii, hataki ku­zungumza na wewe lakini unapomuuliza kama ana tatizo lolote, anakujibu kwamba hakuna tatizo lolote na yupo sawa.

Wengine hudhani kwamba mwanamke husika ameanza dharau, amepata wa­naume wanaompa jeuri au hampendi tena! Kama nilivyosema, ukishindwa kujua hali yake imesababishwa na nini na una­takiwa kufanya nini ili kumrudisha kwenye hali yake ya kawaida, unaweza kujikuta ukisababisha matatizo makubwa zaidi.

Kwa hiyo, jambo la msingi unatakiwa kuwa mwepesi kumsoma mwenzi wako na hii itakusaidia kumgundua muda ambao hayupo sawa. Ukishagundua kama hay­upo sawa na anakuwekea mgomo baridi, muulize kwa upole kama yupo sawa au kama kuna kitu kinamsumbua.

Kwa hiyo unapoona ame­fika katika hali kama hiyo, tambua kwamba kuna ujumbe anataka kukufikishia! Anataka kukuonesha kwamba umem­kasirisha, umemuumiza moyo wake na hafurahishwi na ma­tendo yako.

Unachotakiwa kufanya kwanza ni kutulia lakini pili ni kuanza ku­jichunguza mwenyewe, ni jambo gani umefanya mpaka ukamuudhi? Jiulize mwenyewe ndani ya kichwa chako lakini wakati huohuo, tambua kwamba anahitaji sana ‘attention’ yako.

Mwanamke akinuna, anataka umuoneshe kwamba umeshaelewa kwamba hayupo sawa na unajitahidi kumfanya arudi kuwa sawa! Wengine wanakosea kwamba akishao­na amenuniwa, basi na yeye anaanza visa, a n a a n z a kufokafoka na kuwa mkali, hayo ni ma­kosa.

Unatakiwa kushuka chini hata kama bado hujajua kosa lako ni lipi, kuwa mpole kwake, muoneshe kumjali, jitahidi kujiwe­ka karibu naye na mfanyie mambo mazuri. Kama unajiweza, unaweza hata kumuom­ba mtoke ‘out’, kama amekasirika sana anaweza hata kukataa kutoka na wewe lakini ni jukumu lako kumbembeleza.

Kihulka wanawake wameumbwa kubembelezwa kwa hiyo katika mazingira kama hayo ni nafasi yako ya kuonyesha uwezo wako wa kumbembeleza mpaka akubaliane na kile unachokitaka.

Ukishapata nafasi ya kutoka naye, au hata kama hamjatoka mpo wenyewe ma­hali tulivu, anza kuzungumza naye kwa upole ukitanguliza maneno matamu ya kujishusha na kumuomba akusamehe, bila shaka kama kuna jambo umemuudhi atakueleza kwa uwazi, hata kama unaona siyo jambo la msingi sana, rudia kumuom­ba radhi na mhakikishie kwamba halita­jirudia.

Utashangaa anaanza kurudi kwenye hali yake ya kawaida na lile tabasamu li­lilopotea kwenye uso wake litaanza kuchanua upya. Ukitumia nguvu na ubabe, utakuwa sawa na mtu anayemwagia petroli kwenye moto.
Kwa leo ni hayo tu, tukutane wiki ijayo kwa mada ny­ingine nzuri.
Credit: Global Publishers
MaoniMaoni Yako