Thursday, May 31, 2018

Amber Lulu Aanika Orodha Ya Mastaa Aliowahi Kubanjuka Nao

Tags

Video vixen maarufu nchini Amber Lulu ambaye hivi karibuni amepenya Kwenye tasnia ya Bongo fleva na anafanya vizuri na ngoma yake ya‘Jini kisirani’ ameweka hadharani majina ya wanaume wote aliowahi kubanjuka nao.

Kwenye mahojiano na Clouds Tv, Amber Lulu aliulizwa listi ya wanaume mastaa ambao amesha wahi kubanjuka nao na akawataja hawa: "Barnaba, Aslay, Rammy Galis na Young Dee lakini Young Dee sio sana, hao wanatosha, hao wengine hapana”.

"Aslay nilishatoka naye ila alikuwa ni mtu fulani muelewa, yuko poa, ana heshimu mwanamke. Yuko noma, yuko vizuri, Aslay kiboko kabisa”.Amber Lulu ameiambia Clouds TV.

Amber Lulu alipoulizwa kuhusu Prezzo aliweka wazi  kuwa ni mume wake na anampenda lakini pia Amber Lulu  aliweka wazi kuwa kutokana na video iliyovuja kati yake na Nuh Mziwanda imesababisha yeye Kutoswa na Prezzo.

 by richard@spoti.co.tz