Alikiba aelezea alivyokutana na mke wakeMsanii wa muziki wa Bongo, Alikiba amefunguka namna alivyokutana na mkewe kutokea Mombosa, Kenya na sababu ya usiri katika mambo yake mengi anayofanya.
Muimbaji huyo katika kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV amesema kutokana na safari zake za mara kwa mara nchini Kenya aliweza kukutana naye, pia Gavana wa Mombasa, Hassan Ali Joho alihusika kufanikisha hilo.
“Yeah Joho ni mtu ambaye aliniongoza sana kwenye maswala ya msingi, kama nilivyokuwambia kwenye masuala ya dini, mimi na mke wangu tulikutana Nairobi, tukajuana tukaanza kuwasiliana,” amesema.
“Tulivyokuwa marafiki na Hassan nikamwambia kaka kuna msichana anakaa hapa, akaniambia kama ni kuoa basi process zifuatwe nilipoonja Mo Faya tu!, nikaoa hapo hapo,” amesema Alikiba.
Katika hatua nyingine amesema sababu ya kufanya siri baadhi ya mambo yake kama alivyofanya katika ujio wa kinywaji chake, Mo Faya ni kutokana na kutengeneza shauka ya kutaka kujua zaidi na pia ndio tabia yake.
“Kwa sababu muamko unakuwa mkubwa zaidi wanakuwa hawategemei ni kitu gani Alikiba anaweza akafanya, kwa hiyo kama ni kitu kizuri watu wanakuwa wanafurahi zaidi,” amesema.
Alikiba alioa April 19, 2018 Mombasa nchini Kenya na sherehe ya pili iliyofanyika April 29, Dar es Salaam, Tanzania ndipo alitambulisha rasmi bidhaa yake ya energy drink, Mo Faya. 
Soure: Udaku Secially
MaoniMaoni Yako