Monday, May 21, 2018

Alichokifanya Willian sio cha kiungwana safari kuelekea Man U inakaribia

Tags

Msimu uliopita kulikuwa na habari kubwa sana jinsi Diego Costa alivyoondoka Chelsea, mengi yalisemwa lakini kubwa likiwa ni ugomvi na kutokuelewana kati ya Costa na Conte hadi kufikia hatua Conte kumkataa Costa.
Weekend hii nayo kumeibuka story ya namna hii lakini safari hii ni Conte kufanyiziwa na mchezaji mwingine wa Kibrazil, hii ilikuwa saa chache baada ya Chelsea kutwaa kombe la FA dhidi ya Manchester Unite pale Wembley.
Kupitia katika mtandao wa Instagram mchezaji Willian aliweka picha za matukio wakati wakishangilia ubingwa, lakini gumzo kubwa ni baada ya kuifisha sura ya Antonio Conte kwa kutumia emoji za kombe.
Post hii ya Willian inaonesha kwamba alikuwa akitaka kikosi kizima cha Chelsea kionekane katika picha hiyo kasoro kocha wa timu hiyo na ndio maana akaamua kumuondoa katika picha hiyo kwa kumuwekea emoji.
Willian hakuonekana na furaha alipokuwa amekaa benchi la Chelsea na wakati pekee ambao alionekana akiwa ana furaha ni pale alipokuwa akiongea na kocha Jose Mourinho wa Manchester United
Mashabiki mbali mbali wa Chelsea wamemshambulia Willian kupitia mitandao ya kijamii na kumwambia kama anataka kwenda Manchester United aende tu lakini asilete vitendo vya dharau kwa timu yao.
Source: Udaku Specially