Zlatan hatocheza Kombe la Dunia


London, England. Zlatan Ibrahimovic hatoichezea Sweden katika Kombe la Dunia 2018 baada ya kutangaza kustaafu.
Nyota huyo wa LA Galaxy (36) amesema hivi karibu atakwenda katika mashindano hayo, lakini si kwa sababu ya kucheza.
Kiongozi wa Shirikisho la Soka la Sweden (FA), Lars Richt alisema: "Nimezungumza na Zlatan siku ya Jumanne. Ameniambia kwamba alishatangaza  hatoweza kubadilisha ili acheze timu ya taifa."
Ibrahimovic alitangaza kustaafu soka la kimataifa baada ya fainali za Euro 2016.
Chanzo: Mwanaspoti
MaoniMaoni Yako