Wosia wa Afande kwa wanawe “nikifa msikubali nizikwe, msimamie nichomwe moto”


Msanii wa muziki kutoka mkoani Morogoro, Afande Sele ameacha wosia kwa watoto wake wawili kwamba akifariki wahakikishe anachochwa moto.

Rapa huyo amewata watoto wake wasimamie hilo kwa kuwa hiyo ni zawadi ambayo anaona itamfaa kutokana na malezi kwa watoto wake hao.
“Kila wakati nikipata nafasi ya kuongea na hawa binti zangu wawili huwa nawakumbusha kwamba yote ninayowatendea chini ya jua ni wajibu wangu na ni haki yao lakini kitu pekee kikubwa kwangu wanachoweza kunilipa ni wao kuhakikisha kuwa siku yangu ya mwisho ikifika wasiruhusu kivyovyote mwili wangu kuzikwa/kufukiwa udongoni bali zawadi iliyobora kwangu watakayopaswa kunipa ni kuhakikisha mwili wangu unateketezwa kwa Moto💥 na kubakia majivu ambayo ndio watayazika ardhini na kubakia kama alama ya pale nilipo lala mimi ule usingizi mzito na usiokua na ndoto…’maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua’….usifosi tufanane.
,” aliandika Afande Sele.
Rapa huyo awali aliwahi kutoa taarifa ya kutaka asizikwe na achomwe moto huku akidai hana dini hivyo hataki hausishwe na dini yoyote.
MaoniMaoni Yako