Thursday, April 5, 2018

Watu wasifikiri ninaposafiri nje naenda kufanya starehe – Ommy Dimpoz

Tags

Msanii wa muziki Bongo, Ommy Dimpoz amefunguka undani wa safari zake za mara kwa mara nje ya nchi.

Muimbaji huyo amesema anaposafiri si kwa ajili ya starehe kama watu wanavyoona katika mitandao bali ni kwa ajili ya kazi zake.
“Safari zangu nyingine za nje watu wasifikirie naenda kufanya starehe, ni moja ya kazi kwa hiyo nimerekodi, nika-shoot video kama nne natakiwa ni-shoot nyingine Mwanza next week,” Ommy Diamond ameiambia Bongo5.
Ameongeza kuwa kuanzia October mwaka jana alikuwa anarekodi nyimbo kwa ajili ya albamu yake ambapo amerekodi na producer wa hapa Bongo na wengine ndio amekuwa akiwafuata nje ya nchini.
July 6, 2017 Ommy Dimpoz alijiunga na label ya RockStar400 inayofanya kazi kwa ukaribu na kampuni kubwa ya muziki duniani, Sony Music Entertainment. Muimbaji huyo aliungana na Alikiba ambaye alijiunga na label hiyo miaka sita iliyopita.

by richard@spoti.co.tz