Wasafi TV kuanza kurusha matangazo yake leo

Kituo kipya cha runinga cha Wasafi TV leo Aprili 02, 2018 kitaanza kurusha matangazo yake mubashara kupitia ving’amuzi mbalimbali kikiwemo cha Azam TV.

Akithibitisha taarifa hizo, Diamond Platnumz ambaye ndiye mmiliki na muanzilishi wa kituo hicho, amesema kuwa matangazo hayo yataanza kuonekana kuanzia leo saa moja usiku na kwa watumiaji wa king’amuzi cha Azam, Wasafi TV itapatikana namba 122 .
Nitawatangazie rasmi kwamba kunako majaariwa kesho (Aprili 02, 2018) channel yetu ya Wasafi TV itaanza kuruka rasmi.“amesema Diamond Platnumz jana usiku kwenye ugawaji wa tuzo za Sinema Zetu zilizofanyika jijini Dar es salaam.
Hata hivyo, bado haijajulikana kama Wasafi TV itapatikana kwenye ving’amuzi vingine zaidi ya Azam TV.

by richard@spoti.co.tz
MaoniMaoni Yako