Waithiopia Wtinga Nchini Kwaajili ya Mechi yao na Yanga


Klabu ya soka ya Welayta Dicha ya Ethiopia imetua nchini mchana wa leo, tayari kwa mchezo wake wa hatua ya mtoano kombe la Shirikisho Barani Afrika kuwania kutinga hatua ya makundi.

Welayta imetua na kikosi chake kamili kilichoiondoa Zamalek ya Misri kwenye michuano hiyo hatua ya kwanza na wachezaji wakionekana kuwa na morali kubwa kuelekea mchezo huo.

Timu hiyo inashika nafasi ya 8 kwenye msimamo wa ligi ya nchini kwao ikiwa na alama 23 katika mechi 17. Mchezo unatarajia kupigwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam April 7.

Kwa upande wa Yanga yenyewe imeweka kambi mkoani Morogoro kwaajili ya mchezo huo na itarejea Dar es salaam kesho Alhamisi tayari kwa mchezo huo ambao kama itautumia vizuri itarahisisha kazi ugenini wiki mbili zijazo.
Chanzo: Udaku specially
MaoniMaoni Yako