Wachezaji hawa wanne wa yanga kukosa mechi ya CAF


Wakati zikiwa zimesalia siku kadhaa kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, Yanga itawakosa wachezaji wake kadhaa.
Yanga itakuwa nyumbani Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kucheza dhidi ya Welayta Dicha FC kutoka Ethipia.
Katika mchezo huo, Yanga itawakosa wachezaji Papy Tshishimbi, Obrey Chirwa, Said Makapu pamoja beki Kelvin Yondani ambao wanatumikia adhabu ya kadi za njano.
Wapinzani hao wa Yanga wanatarajiwa kuwasili mchana wa leo majira ya saa sita, jijini Dar es Salaam  

Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz
MaoniMaoni Yako