Wachezaji hawa 7 wataondoka Simba Chirwa alengwa


Wachezaji takribani Saba (7) wa Vinara wa Ligi Kuu Simba SC kuondoka Mwishoni mwa Msimu huu,wengi wao Mikataba inamalizika na tayari wameonesha nia ya kutaka kuondoka Klabuni hapo pia Wengine Kukosa Nafasi ya Kucheza kunawafanya kuanza kutafuta timu nyingine kwa Msimu Ujao. Mohammed Ibrahim "MO" Ambaye Ameripotiwa kuwa na mahusiano Mabaya na benchi la Klabu yake kilichopelekea kushindwa Kucheza Msimu huu. Kiungo huyo Mshambuliaji ni Mmoja ya Wachezaji Ambao hawatabakia Simba SC Msimu Ujao.
 
Wengine ni Juma Luizio Ambaye mfumo mpya wa kocha Piere Lechantre Umemfanya kusugua benchi pia Laudit Mavugo nae kukosa Navas ya Kucheza tofauti na Msimu Uliopita Ujio wa John Boco na Emmanuel Okwi Unamfanya kusubiri Mmoja wao haumie au kocha Ampumzishe na yeye ndio Achukue Nafasi Akitokea benchi. Mkongwe Mwinyi Kazimoto Ambaye Umri Umeenda Miaka 34 Sasa na Ameripotiwa kuwa Anastaafu Soka Ifikapo Mwisho wa Msimu huu.

 Wachezaji Wengine Ambao Klabu ya Simba SC inapenda kuwapa Mikataba mipya lakini kukosa kwao Nafasi za Kucheza ndio Sababu Inayopelekwa Wao kuhiama Klabu hiyo ya Mitaa ya Msimbazi. Wachezaji hao ni Mohammed Hussein "Tshabalala",Jamal Mwambeleko na Paul Bukaba.... Pia kuna Wachezaji Ambao Wanamaliza Mikataba yao ndani ya Simba SC na Mpaka Sasa hakuna Maongezi juu ya kuwasainisha Mikataba Mipya. Hao ni Winga Matata Shiza Ramadhan Kichuya Ambaye Vilabu Mbalimbali nje ya Nchi Vimeanza kusaka Saini yake Vikiwemo kutoka Misri pia DR Congo Miamba ya Nchini humo TP Mazembe...

.Mwingine ni Kiungo Mzamiru Yassini. Licha ya kuhusishwa kuondoka kwa Wachezaji hao Klabu ya Simba SC Imeanza kutafuta saini za Baada ya Wachezaji kuziba Nafasi zao. Adam Salamba wa Lipuli FC anatajwa kuwindwa na Simba SC, Obrey Chirwa wa Yanga SC, Mchezaji huru Mudathir Yahya na kusajili Wachezaji Wengine kwa Ajili ya Mashindano ya Kimataifa Ambapo Mpaka Sasa Wana Uhakika wa Kushiriki. 
Na: Agape Patrick 
Email: agape@spoti.co.tz
Source: Sokaplace 
MaoniMaoni Yako