Ushauri wa Matola “Simba iamke ikitaka kushinda mechi ya Yanga”

mchezaji wa simba emmanuel okwi akijaribu kumtoka mchezaji wa lipuli.. ( picha na Lebab)
Kocha msaidizi wa Lipuli Selemani Matola amesema alikuwa anaiogopa Simba lakini timu hiyo imecheza chini ya kiwango dhidi ya timu yake kuliko mechi zote za ‘mnyama’ zilizopita.

“Nilikuwa naiogopa sana Simba lakini nimeona imecheza chini ya kiwango dhidi yetu, sio Simba ambayo nimeiona ikicheza kwenye game zilizopita.”
“Sio kwamba tuliwakamia, leo walikuwa chini sana tofauti na mechi zao zote ambazo wamecheza.”
“Kikubwa ni kwamba sisi tunataka kumaliza katika nafasi za juu angalau nafasi ya tano au ya sita kwa hiyo tumejipanga kuhakikisha tunashinda kila mechi tunayokutana nayo.”
Matola ambaye alicheza Simba na baadae kuwa kocha msaidizi kabla ya kujiuzulu ameishauri Simba kuinua kiwango chake kama inahitaji kushinda mechi dhidi ya Yanga Aprili 29, 2018.
“Kama kweli wanataka kushinda game yao dhidi ya Yanga wanatakiwa waamke kwa sababu kiwango chao kilikuwa chini sana.”

posted by Lebab
chanzo: Spoti Tz1
MaoniMaoni Yako