Ukimuuliza manara kuhusu mkude kama atacheza leo

Afisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, amesema kikosi cha Simba kimefanya mazoezi ya mwisho leo kuelekea mchezo wa ligi dhidi ya Njombe Mji FC kesho.

Akizungumza na kipindi cha EFM kupitia E Sports jioni hii, Manara amesema tayari wameshajiandaa kikamilifu na watajitahidi kupata alama tatu muhimu kwenye mchezo huo.

Manara ameeleza pia suala la kiungo Jonas Mkude kuanza kesho kwa kusema kuwa itakuwa ni maamuzi ya Kocha wa timu, japo kwa mujibu wa Daktari hali yake iko vizuri.

"Hali ya Mkude iko vizuri lakini suala la kucheza kesho ni juu ya maamuzi ya Mwalimu" alisema.

Mkude alianza mazoezi jana wakati kikosi kikiwa Iringa katika Uwanja wa Samora chini ya Daktari wa timu, Yassin Gembe,

Source: Saleh Jembe
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz
MaoniMaoni Yako