Tunda Kufunga Ndoa na Casto Dickson Mwaka Huu


Mtangazaji wa Siz kitaa ya Clouds Tv anatarajia kufunga ndoa na video queen maarufu Tunda ambae wamekuwa katika mapenzi kwa muda sasa.Casto anasema kuwa kabla ya mwaka huu kuisha lazima atamuoa mwandada huyo.

"Unajua nimekuwa na wanawake tofauti sana lakini kwa tunda nimekuta vitu tofauti sana,kwangu naona anafaa kuwa mke wa mtu tofauti na watu wa nje mnavyomuona. na nitamuoa kabla ya huu mwaka haujaisha."

Kuhusu kuwa na mwanamke aliyepita katika mahusiano na wanaume wengi, Casto anasema kwake yeye anaanzia pale alipoanza na Tunda na wala haangalii kule nyuma alkopita kwa sababu hata yeye pia alishakuwa na wanawake wengi.

"Alafu kila unapokuwa na mahusiano na mwanamke na ukataka kujua wanaume alikuwa nao yatakushinda.unachotakiwa kuangalia ni pale mnapoanzia tu. Kwani hata mimi nilishakuwa nao wengi tu kabla ya lukutana na Tunda.
MaoniMaoni Yako