TIBOROHA: Simba msiibeze Yanga


Katibu Mkuu wa zamani wa Yanga, Dokt. Jonas Tiboroha, amewasihi Simba kutoibeza Yanga kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi yao, utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Jumapili ya wiki hii. Simba na Yanga zitakutana katika mechi hiyo inayosubiriwa na umati lukuki wa mashabiki wa soka la Tanzania nchini. Tiboroa ameeleza kuwa msimu huu Yanga haijafanya vizuri kama Simba ambayo imeonekana kuwa ina kikosi kipana. Katibu huyo wa zamani wa Yanga ameeleza pia uzuri wa Simba usiwafanye wajiamini zaidi kuelekea mechi hiyo ambayo huwa si rahisi kutabirika pindi vigogo hawa wanapokutana. "Unajua timu hizi zinapokutana si rahisi kutabirika, Simba wapo vizuri msimu huu, wana kikosi kipana, lakini hawapaswi kuibeza Yanga kwa maana yeyote yule anaweza akapata matokeo.
  Na: Agape Patrick Email: agape@spoti.co.tz
Source: Saleh Jembe
MaoniMaoni Yako