Tetesi Za soka Barani Ulaya leo Ijumaa 27/04/2018

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anasema kuwa anahitaji sifa kwa kumleta Chelsea mshambuliaji wa Misri mwenye umri wa 25 Mohamed Salah wakati alipokuwa mkufunzi wa Chelsea na sio lawama ya kumuuza mchezaji huyo katika klabu ya Roma 2016. (ESPN)
Tottenham iko tayari kumuuza beki wake wa kushoto Danny Rose, 27, beki wa kati wa ubelgiji Toby Alderweireld, kiungo wa kati wa Kenya Victor Wanyama, 26, na kiungo wa kati wa Ubelgiji Mousa Dembele kuchangisha £170m huku mkufunzi Mauricio Pochettino akitarajiwa kuimarisha kikosi chake kwa msimu ujao. (Mail)
Mkufunzi wa Leicester City Claude Puel anapigania kuokoa kazi yake katika klabu hiyo huku timu hiyo ikipanga kufanya mabadiliko makubwa ya kikosi chake mwisho wa msimu huu.. (Telegraph)
Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale amekasirishwa na hatua ya klabu hiyo kutomchezesha mara kwa mara lakini kuna wasiwasi wa iwapo kuna klabu ya Uingereza itakayoweza kumnunua mchezaji huyo. (Guardian)
Arsenal itashindana na Atletico Madrid na Napoli katika kumwania kipa wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Bernd Leno, ambaye anapatikana kwa dau la £17.5m. (Bild via Sun)
West Ham wamejiunga katika mbio za kumsajili beki wa Ireland Kaskazini Jonny Evans kwa dau la £3m huku timu hiyo ya ligi ya Premia ikijiandaa na kushushwa daraja kwa West Brom(Mirror)
Kushindwa kwa mkufunzi wa Everton Sam Allardyce kupata uungwaji mkono kutoka kwa mmiliki wa klabu hiyo Farhad Moshiri kumefanya hatma ya kocha huyo kutojulikana (Mail)
Kiungo wa kati wa Brazil Andreas Pereira ataondoka Manchester United mwisho wa msimu huu iwapo mchezaji huyo mwenye urmi wa miaka hatapewa hakikisho kuhusu kushiriki katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo.(Telegraph)
Mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich amewataka wafanyi kazi kupigania mipango ya uhamisho licha ya hatma ya kocha Antonio kutojulikana , ikiwemo uhamisho wa kiungo wa kati wa Nice na Ivory Coast Jean-Michael Seri kwa dau la £30m. (Mirror)
Mkufunzi wa zamani wa Barcelona Luis Enrique, anayepigiwa upatu kumrithi mkufunzi wa Arsenal anayeondoka Arsene Wenger katika klabu ya Arsenal, anataka kitita cha £200m kuimarisha kikosi cha The Gunners msimu ujao. (Sun)
Mkufunzi asiyetaka masikhara kama vile kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone, anahitaji kumrithi Wenger katika uwanja wa Emirates ,kulingana na kiungo wa kati wa Ireland Andy Townsend. (BBC Radio 5 live)
Manchester United wameishinda Liverpool na Chelsea katika kumsajili kiungo wa kati Martin Svidersky, 15. Raia huyo wa Slovakia, ambaye amekuwa akicheza soka ya vijana alikuwa akivutia hamu kutoka Manchester City na West Ham.(Mail)
Beki wa zamani wa Uingereza, Tottenham na Arsenal Sol Campbell anatarajiwa kufanya mazungumzo na Ipswich Town huku wakitafuta kumrithi Mick McCarthy. (Telegraph)

Source:bbc swahili
MaoniMaoni Yako