Tetesi Za Soka Barani Ulaya leo Alhamisi 26/04/2018

Liverpool itazuia hamu yoyote kutoka kwa Real Madrid ya kutaka kumnunua mshambulaji wa Misri Mohamed Salah, ambaye wanasema ana thamani ya £200m. (Mail)
Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Roma Monchi ametetea uuzaji wa Salah kwa Liverpool, akisisitiza kuwa klabu hiyo ya Itali haikuwa na chaguo kutkana na matatizo ya kifedha.(Guardian)
Mkufunzi wa Atletico Madrid Diego Simeone anasema kuwa hana mawasiliano yoyote na Arsenal kuhusu kazi ya ukufunzi ya klabu hiyo kufuatia tangazo la mkufunzi wake Arsene Wenger kwamba anaondoka mwisho wa msimu huu.Mirror)
Mkufunzi wa New York City Patrick Vieira angependelea kurudi Arsenal wakati mkufunzi Arsene Wenger atakapoondoka mwisho wa msimu huu na kuongezea kwamba yuko tayari kufunza Ulaya.(Times)
Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale huenda akahamia Bayern Munich mwisho wa msimu huu , lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 anasema kuwa lengo lake kuu ni kuisaidia Real Madrid kushinda mataji. (Bild, via Independent)
Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho amejiandaa kumuachilia mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 22, kuondoka mwisho wa msimu huu (Tuttosport, via Manchester Evening News)
United inalenga kumshawishi beki wa klabu ya Fulham Ryan Sessegnon 17 kuhamia Old Trafford. (Times)
Arsenal huenda ikashindana na wapinzani wake katika ligi ya EPL Manchester United na Chelsea kwa usajili wa kiungo wa kati wa Roma na Ubelgiji mwenye umri wa miaka 29 Radja Nainggolan. (Sun)
Manchester City na Manchester United zote zinamnyatia kiungo wa kati wa Napoli na Itali mwenye umri wa miaka 26-Jorginho. (Star)
Tottenham inataka kuwasajili wachezaji watatu wa Ureno mwisho wa msimu huu -winga wa Sporting Lisbon Gelson Martins, 22, beki wa kulia wa Southampton Cedric Soares, 26, na kiungo wa kati wa Wolves Ruben Neves, 21. (Mirror)
Source:bbc
MaoniMaoni Yako