Tetesi za soka barani ulaya leo Jumanne tar 03/04/2018


  • Kipa wa timu ya Manchester United, David de Gea (27) anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka tano inayo na thamani ya paundi £350,000 kila wiki. (Sun)

  • Timu ya Tottenham wanamatumiani kuwa meneja Mauricio Pochettino na wachezaji sita wakuu watasaini makubaliano mapya katika miezi michache inayokuja (Telegraph)

  • Timu ya Paris St-Germain wakotayari kumpatia mlinzi Tottenham Toby Alderweireld, 29, mkataba anaoutaka wa paundi milioni 10m-kwa kila msimu kwa miaka mitano wakati Mbelgiji huyo anatarajiwa kuondoka Spurs baada ya mazungumzo kuhusu makubaliano mapya kuisha. (Mail)

  • Meneja wa Manchester City Pep Guardiola atakuwa na timu dhaifu dhidi ya mechi na Manchester United Jumamosi hii, ambapo kwa kishindo ingewapatia tuzo ya Premier League. (Express)
  • Derek McInnes, Craig Shakespeare, Michael Appleton, Dean Smith na Graham Potter wako katika orodha ya kuchaguliwa kuwa meneja wa West Brom  katika majira ya joto. (Times)
  • Mmiliki wa timu ya Chelsea Roman Abramovich hajafurahishwa na jambo la klabu kukosa kucheza katika ligi ya Champions lakini anasita kumfuta kazi meneja Antonio Conte,ambaye amebakia na mwaka mmoja katika mkataba wake wenye thamani ya paundi milioni 9.5.(Express)


  • Chelsea wanakabiliana na uwezekano wa kuwapoteza wachezaji tisa katika kikosi cha kwanza majira ya joto (Telegraph)
  • Mlinzi wa Uhispania na Chelsea Marcos Alonso, 27, anasema kuhangaika kwa timu yake msimu huu imesababishwa na wao kukosa 'uendelevu' na 'bahati' uliowasaidia awali kuchukua tuzo ya ligi ya Premiere msimu uliopita. (Star)
  • Liverpool wanamatumaini ya kumpata Valencia Ferran Torres, ikiwa pia timu ya Chelsea  wanamtaka kijana huyo wa umri wa miaka 18 (Mail)
  • Everton itatakiwa kukabiliana na vilabu vitatu vya Uhispania kama wakitaka kumpata mlinzi Wilfried Kanon kutoka Ivory Coast (Sun)
Source:bbc
MaoniMaoni Yako