Simba yalimwa faini, Singida yapata pigo


Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, Boniface Wambura, alisema jana baada ya kikao cha Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi (Kamati ya Saa 72) kumalizika kuwa Simba imepigwa faini ya Sh. 500,000 kutokana na kuonyesha vitendo vinavyoashiria ushirikina katika mechi yake dhidi ya Njombe Mji iliyofanyika kwenye Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe
Lipuli wakicheza na Simba

Wambura alisema pia shabiki mmoja wa timu hiyo ya jijini Dar es Salaam aliingia uwanjani na kuchukua taulo la kipa wa Njombe Mji lililokuwa golini na kueleza kuwa adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 42(1) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Klabu.
Alisema pia Simba imepigwa faini ya Sh. 500,000 kutokana na mashabiki wake kuingia uwanjani baada ya filimbi ya mwisho baada ya mechi dhidi ya Mtibwa Sugar na faini nyingine ya Sh. 500,000 ni kwa sababu ya kuwakilishwa na maofisa watatu badala ya wanne katika kikao cha maandalizi ya mechi dhidi ya Prisons iliyofanyika jijini.  
Aliongeza kuwa pia mshambuliaji wa Singida United, Tafadzwa Kutinyu, amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya Sh. 500,000 kutokana na kufanya vitendo vyenye kuonyesha imani za ushirikina katika mechi hiyo iliyochezwa Aprili 6, 2018 kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida.
"Kutinyu alichukua taulo la kipa wa Mtibwa Sugar na kulirusha jukwaani kwa mashabiki wa Singida United ambao waliondoka nalo," ilisema sehemu ya taarifa ya bodi hiyo ya ligi.
Pia Klabu ya Mbao imepigwa faini ya Sh. 500,000 kutokana na mashabiki wake kuingia uwanjani na kuchukua glovu za akiba za kipa wa Lipuli zilizowekwa golini na kukimbia nazo, kitendo kinachoonyesha imani za kishirikina.
 Chanzo:IPP Media
MaoniMaoni Yako