Powered by Blogger.

Slider

Breaking

MICHEZO

HABARI

MAGAZETI

UDAKU

BURUDANI

VIDEOS

» » Simba ‘ikikaza’ kidogo tu safi!


KIRAKA wa Simba, Shomari Kapombe ni miongoni mwa wachezaji wachache waliokuwepo wakati Wekundu hao wakitamba kimataifa kabla ya kupotea na kubatizwa jina la ‘Wamatopeni’.
Sasa jamaa ameapa kuwa, kwa uzoefu alionao kama wachezaji wote watakaza kidogo tu basi ubingwa msimu huu unatua Msimbazi.
Pia, amesema kwa hali ilivyo kwa sasa hawataki kupoteza mchezo na kwamba, kila mechi kwao ni fainali.
Kapombe, ambaye aliichezea Simba 2011 hadi 2013 kabla ya kutimkia Ufaransa na baadaye kurudi wakati Simba ikipoteza mwelekezo na kushindwa kubeba mataji.
Sasa Kapombe amekiangalia kikosi chao na kusema, kuna wachezaji wengi mahiri na wenye uwezo mkubwa kuhimili ushindani hivyo wana uhakika wa kubeba taji.
“Nina uzoefu wa kutosha najua nyakati pia, kwa timu ambayo tuko nayo tuna kila sababu ya kuwa mabingwa. Kuna wachezaji wenye uzoefu wa kutisha kila mmoja akiwa amecheza si chini ya misimu minne na morali ipo juu akitamani ufalme huo,” alisema Kapombe ambaye alirudi nchini mwaka 2014 akajiunga na Azam na 2017 akarudi tena Simba anayoichezea sasa.
“Ligi ni ngumu lakini unaona Simba inapambana kusaka ubingwa na jambo la muhimu ni kutodharau mechi zote kuanzia sasa hadi tunamaliza ligi,” alisema.
Simba ndiyo vinara wakiongoza na pointi 49 kisha Yanga yenye pointi 46, Azam 44, Tanzania Prisons ni wa nne wana 36 sawa na za Singida United wanaoshika nafasi ya tano na majanga yako kwa timu za Majimaji, Njombe Mji na Mbao FC ambao wanapishana kwenye nafasi za mkiani.
Simba imebakiza michezo na Mtibwa kesho Jumatatu, Yanga, Singida United, Mbeya City, Tanzania Prisons, Ndanda, Kagera Sugar, Lipuli na Majimaji.
Chanzo: Mwanaspoti

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post