Sikukuu ya wajinga yamchanganya etoo mbioni kukimbilia mahakamani


Juzi kulikuwa na habari katika moja ya majarida nchini Cameroon kuhusiana mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon Samuel Etoo kujiandaa kugombea uraisi wa nchi hiyo mwaka 2018.
Jarida lililofahamika kama Young Africa Magazine lilichapisha habari hiyo siku ya tarehe 1 na gumzo kubwa sana nchini Morocco lakini kumbe habari hii haikuwa ya kweli bali ilikuwa ni siku ya wajinga.
Baaada ya jarida hilo kuchapisha habari hiyo ilianza kusambaa kwa kiasi kikubwa sana kiasi cha vyombo vya habari nchini Ufaransa kuanza kuiandika habari hiyo na wakisema chanzo ni jarida hilo la Cameroon.
Samuel Etoo kwa upande wake amekasirishwa vibaya sana na habari hii na kupitia mtandao wake wa Face Book ameweka wazi hasira zake kutokana na tukio hilo na anapanga kwenda mahakamani kulishtaki jarida hilo.
“Nimesikitishwa sana na muandishi wa habari hii, uchaguzi wa Cameroon ni zoezi serious sana na halipaswi kujadiliwa kirahisi hivyo, ninaheshimu nchi yangu sana pamoja na watawala wake” hayo ni baadhi ya maandishi katika ujumbe wa Etoo.
Baadae jarida hilo liliomba radhi na kutoa taarifa kwamba habari ilitolea tarehe ambayo ni siku ya wajinga, bado Etoo hajaweka wazi moja kwa moja kama atalichukulia jarida hilo hatua au laa lakimi tayari ameanza kuongea na wanasheria wake kuhusu hatua za kuchukua.
Source: Shaffih Dauda
Na: Agape Patrick
Email: agape@spoti.co.tz
MaoniMaoni Yako