Shuhudia Viti Vya Magari vilivyotengenezwa kwa Vitenge


Mjasiriamali kijana kutoka nchini Uganda Christine Namubiru Mutebi ni muanzilishi mwenza wa kampuni iitwayo 1620 Footsteps. Amepata ufanisi mkubwa kwa kuyaremba magari ndani kwa kutumia vitambara vya kiafrika kama vitenge.

Huu ni ubunifu wa hali ya juu, alipoulizwa ilikuwaje akaja na wazo hilo, alisema " maisha yamekuwa ni magumu na mimi kama kijana niliwaza ni kwa jinsi gani naweza kujikwamua, ndipo nilipogundua kwamba kuna wamiliki wa magari ambao wangetamani magari yao yawe na muonekano wa ki Africa zaidi, na hivyo kufikiria ni kitu gani basi kinaweza kufanya muonekano huo, ndipo nikaja na wazo hili."