Serengeti Boys Haooooooooooo Fainali CECAFA

MABAO mawili yaliyofungwa na Jaffar Juma na Kelvin Paul yameivusha timu ya Taifa ya Vijana U17 ya Tanzania, 'Serengeti Boys' na kutinga fainali ya michuano ya CECAFA baada ya kuing'oa Kenya hatua ya nusu fainali kwa mabao 2-1.
Serengeti Boys ambayo imecheza mchezo huo  kwenye Uwanja wa Muyinga nchini Burundi, umeifanya Serengeti kuifuata Somalia waliowavua taji waliokuwa watetezi Uganda kwa kuifunga bao 1-0 katika mchezo mwingine uliochezwa pia leo Jumatano.
Mechi hiyo ya fainali itachezwa Jumapili na keshokutwa Jumamosi Uganda itavaana na Kenya kumtafuta mshindi wa tatu.
Source:Mwanaspoti
MaoniMaoni Yako