SEMENYA: Atakiwa kupunguza Homoni zake za Kiume kama Anataka kwenda huku..

Caster Semenya


Caster Semenya, mwanariadha wa Afrika ya Kusini, anaetawala katika kipengele cha Mbio fupi za wanawake anaweza kufikia mwisho wa utawala wake baada ya sharia mpya yenye vigezo vipya kuanzishwa . Kutokana na sharia hiyo mpya, Semenya atatakiwa kupunguza  HOMONI zake ambazo nyingi ni za kiume katika mwili wake, kama inavyofahamika kwamba Semenya ana vinzsaba vya Jinsia mbili.

Hivyo basi Semenya na wanariadha wengine wenye aina hiyo ya miili wanatakiwa kufanya jitihada za kupunguza HOMONI hizo ikiwa wanataka kushiriki katika mashindano ya Olympic na Mashindano ya dunia.

MaoniMaoni Yako