Salah Anyakua Tuzo ya Mchezaji bora wa Mwaka EPL 2017/18


Mohamed Salah ametawazwa kuwa mshindi wa tuzo ya Mchezaji bora wa Mwaka wa EPL Jana Juma Pili 22/04/2018. Hii inatoka na ukweli kwamba Salah hadi sasa ndie mfungaji hatari anayeongoza kwa magoli ya kufunga katika ligi hiyo, amepata tuzo hiyo huku akiwa na idadi ya magoli 31
Mohamed Salah

“Ni heshima kubwa sana kwangu, nimekuwa najituma sana na kufanya kazi kwa bidii sana, nina furaha kweli kwa kupata tuzo hii.” Salah aliyasema hayo kwenye hafla iliyoandaliwa siku ya Juma Pili jioni.

“Unalinganisha jina lako na baadhi ya wachezaji wakubwa  maana kuvunja records katika Ligi ya EPL siyo jambo dogo, ni jambo kubwa kabisa hapa Uingereza na Duniani kote, nab ado kuna michezo mitatu hakika nataka kuweka historia mpya” Aliongeza Salah

Mbali na mafanikio hayo ya Salah katika ligi ya EPL, bado ana idadi nzuri a magoli katika ligi ya UEFA,
Kocha wa Manchester City ametoa maoni yake kuhusu Tuzo hiyo ya Salah: “Kwa mawazo yangu ukiwa unachambua wachezaji wazuri katika miezi 10, hakuna mchezaji anayemzidi Salah” alisema Guardiola.

sabby@spoti.co.tz


MaoniMaoni Yako