Real Madrid Kumsajili Mohamed Salah


REAL Madrid imemfanya staa wa Liverpool, Mohamed Salah kuwa chaguo la kwanza klabuni hapo katika dirisha kubwa la usajili la majira ya joto na wapo tayari kutoa dau la Euro 200 milioni kwa ajili ya staa huyo wa kimataifa wa Misri.
 Salah alichaguliwa kuwa mwanasoka bora wa England msimu huu na anapewa nafasi kubwa ya mfungaji bora wa Ligi kuu ya England msimu huu mbele ya Harry Kane wa Tottenham Hotspurs na sasa Perez amefanya chaguo la kwanza kutua Santiago Bernebeu.
Perez ana wasiwasi na kikosi chake ambacho kimeendelea kuzeeka msimu huu huku wachezaji wengi wakishindwa kuonyesha ubora wao kiasi cha kupigwa bao na Barcelona katika michuano mbalimbali ya ndani ya Hispania.
Tujiandae kusikia kelele za "Moo Salah, Moo Salah, the Egyptian King" katika uwanja wa Madrid.
MaoniMaoni Yako